March 27, 2018

Tambua tabia hizi na uhusiano wake na kisaikolojia.

1:Mtu ambaye ametendwa au ameumizwa kisaikolojia huwa na hulka ya kukasirika pasipo sababu ya msingi.

2:Ukitaka kujua kama mtu unayezungumza nae anapenda kusikia unayoyazungumza kunja mikono yako,kama anapenda na anafurahia mazungumzo nae atakunja mikono.

3:Kama mtu anachekacheka tu bila sababu maalumu au anacheka sana, basi mtu huyo ana huzuni kuu moyoni mwake, na kama mtu analala Kwa mda mrefu sana, mtu huyo ni mpweke.

4:Namna tunayozungumza na watoto wetu ndivyo inavyokuwa sauti katika mioyo yao.

5:Mtu akitokea katika ndoto unayoota, basi ni Kwa sababu mtu huyo kakuhamu (kakumisi)

6:Wa kwanza kuomba msamaha siku zote ni mwerevu, wa kwanza kusamehe ni mwenye nguvu na wa kwanza kusahau ni mwenye furaha.

7:Ukitumia mkono wako usiotumika mara Kwa mara (wa  kushoto Kwa wengi) itakusaidia kuwa na  ‘self -control ‘

8:Mwanaume akiwa hajisikii huru au akiwa hana amani basi hushika kichwa au uso wakati mwanamke hushika ama nywele,hereni,mavazi,mikono au shingo.

9:Aina mbili ya watu ambao hawatakuangalia machoni ni, mtu anayejaribu kuficha uongo na mtu anayejaribu kuficha upendo.

10:Wanasaikolojia wanasema, mtu anayetaka kumfurahisha kila mtu huishia Kuwa mpweke zaidi.

11:Mtu anayekasirika kirahisi, kwa vitu vya kijinga, inaonesha kwamba anahitaji kupendwa (upendo)

12:Kulia ni afya kwako. Huondoa bakteria wabaya mwilini mwako. Hukupunguzia msongo wa mawazo na kukuongezea kinga ya mwili.

13:Saikolojia inasema :kujifanya mwenye furaha wakati una maumivu ni mfano wa  kuonesha jinsi gani wewe ni mwanadamu mwenye nguvu(strong person)

14:Kabla ya kulala asilimia 90 ya akili yako huanza kufikiri mambo ambayo ungependa yatokee.

15:Watu wanaotembea Kwa hatua za haraka haraka huonekana kuwa wanajiamini na wenye furaha zaidi kuliko wanaotembea taratibu.

16:Kufuatana na uchunguzi wa wataalamu, kumtamani mtu kingono huishia miezi minne, zaidi ya hapo utakuwa ni upendo wa dhati.

17:Uchunguzi unaonesha kuwa watu wanaolala na mito mingi ni wenye msongo es mawazo na wapweke.

18:Watu wakiwa kwenye kundi na ikatokea kuna   kucheka,wale walio na mahusiano ya karibu zaidi huangaliana, kutizamana.

19:Kwa namna mwandiko wa mtu unavyokosa mpangilio au Kuw√° mbaya ndio kiashiria kwamba mtu huyo anafikiri haraka zaidi ya mikono yake inavyoweza kuandika.

20:Haiwezekani kukaa na hasira dhidi ya umpendae Kwa mda mrefu, hasira inayofika siku tatu au zaidi inamaanisha kwamba hauna upendo.

21:Kama mtu akiongea na wewe halafu kwenye maongezi akakuangalia machoni Kwa asilimia 60 ya maongezi basi umemboa mtu huyo. Kama atakuangalia Kwa asilimia 80 basi umemvutia mtu huyo na kama itafikia asilimia 100 basi mtu huyo anakutishia.

22:Unapopiga chafya unakufa Kwa sekunde.

23:Kukosa usingizi husababisha ubongo kutokumbuka mambo kiusahihi.

24:Unapotekenywa hucheki, bali ni itikio la kupaniki (Panic-response). Huwezi jitekenya mwenyewe Kwa sababu mwili hauhisi hatari yoyote. Kawaida enzi za zamani kutekenya ilitumika kama adhabu.