March 14, 2018

Tambua umuhimu wa maji mwilini.

maji ni sehemu ambapo shughuli za kimetaboliki hufanyiki.
Maji katika mwili yanasaidia kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kimetaboliki zinafanyika katika mwili mwako, hurahisisha umeng'enyaji wa vyakula katika mwili wako, kiafya unashauriwa kunywa maji kabla au baada ya kula chakula chakoo ila shughuli za umeng'enyaji chakula chako uweze kufanyika kiurahisi zaidi;

maji yanasaidia kusawazisha joto la mwili wako.
Maji katika mwili yasaidia kuupoza mwili endopo joto la mwili likiwa limezidi maji yanaweza kutumika kama kuupoza mwili kwa joto kali lilipo katika mwili either kwa kuyanywa au kuyaogaa;


maji husaidia kuyeyusha mafuta yaliyo ganda pembeni mwa mishipa ya damu.
Matumizi ya maji haswa yale ya vuguvugu yanasaidia kuyeyusha mafuta yaliyoganda pembeni mwa mishipa ya damu ambayo husafirisha damu sehemu mbalimbali za mwili, ambapo hayo mafuta yakizidi hupelekea magonjwa ya moyo;

maji husaidia usafirishaji wa virutubisho mbalimbali katika mwili.

Maji husaidia kusambaza virutubisho mbalimbali katika mwili vilivyo meng'enywa, hivyo kupitia maji virutubisho vingi vinaweza kufika sehemu mbalimbali za mwili;

maji husaidia utoaji wa sumu katika mwili.

Maji husaidia utoaji wa sumu mbalimbali mwilini kupitia utoaji wa jasho na mkojo, kiwango cha maji kinacho hitajika katika mwili kinapopungua ndipo mtu huhisi kiu ya maji, lakini kiafya unashauriwa kunywa maji hatakama hauna kiu ya maji.