March 12, 2018

Ufilipino wamejenga kisiwa kwa ajili ya wanawake tu.

Usawa wa kijinsia na mambo yanayoendana na hayo ni agenda ambayo inazungumzwa duniani kote lakini ni suala kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea lengo likiwa kuwapa wanawake nafasi ya kufurahia haki zao.
Nchini Ufilipino wamepiga hatua zaidi kwenye masuala ya kuwezesha wanawake ambapo, kisiwa kipya cha wanawake tu kinajengwa, lengo kuu ikiwa ni kutengeneza sehemu ambapo wanawake wa nchi hiyo watakwenda kupumzika na kufurahia.
Kisiwa hicho kiitwacho SuperShe kinamilikiwa na binti ajulikanaye kama Kristina Roth,ambaye ni Mjasiriamali na Mwanzilishi wa blog ya mitindo ya maisha na mtandao iitwayo Supershe.
Kisiwa hicho kikianza kutumika, itamuhitaji mwanamke anayetaka kwenda kutembelea alipe Dola za Marekani 3,500 sawa na Shilingi za Tanzania Milioni 8.4 kwa kipindi cha wiki moja na inaelezwa kuwa kisiwa hiki kitazinduliwa rasmi mwaka huu 2018.