March 2, 2018

Unataka mtoto wako afanye vizuri darasani? Hivi ni vyakula vya kumpa.

Wazazi hufanya kila wanaloweza kuwasaidia watoto wao wafanye vizuri darasani.

Huenda utafiti huu mpya unaweza kuwasaidia wazazi kuwafanya watoto wao wawe vichwa zaidi darasani.

Watoto wanaokula matunda, mboga za majani na samaki katika miaka mitatu ya mwanzo ya shuleni, hufanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuliko wenzao wanaokula chakula kisicho na lishe, utafiti umebaini.

Utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Eastern Finland, ulidai kuwa chakula bora huwa na faida kubwa katika ubongo. Ulifanywa kwa kuhusisha watoto 161 wa kuanzia miaka sita hadi nne na kuwafuatilia kuanzia wakiwa darasa la kwanza hadi la tatu.

Ubora wa chakula chao uliangaliwa kupitia rekodi za walichokula, na ujuzi wao kitaaluma kwa usaidizi wa majaribio ya darasani.

Utafiti huo ulionesha kuwa watoto ambao mlo wao ulikuwa na mboga za majani, matunda na samaki kwa wingi, mafuta kidogo na sukari kwa mbali, walifanya vyema kwenye majaribio.