March 17, 2018

Usipambane na watu ,pambana na maono yako toka kwa Mungu.

Nimetafakari sana Aina ya maisha yetu hapa Duniani, yamejaa Makwazo, Misukosuko, fitina na hila, miongoni mwayo ni mambo machache sana yanatoka kwa Shetani, ila Mengi tunatendewa na Ndugu zetu, jamaa na Marafiki tunaoishi nao katika Jamii.

2 Samueli:5.10 
Naye Daudi akazidi kuwa mkuu; kwa maana Bwana, Mungu wa majeshi, alikuwa pamoja naye.

Bwana Yesu asifiwe sana sana.

Hii ni moja ya kanuni muhimu sana katika maisha yako kama unataka kufikia viwango vya juu kabisa ambavyo Mungu amekukusudia tangu ukiwa tumboni mwa mama yako.

Naongea na mtu mwenye maono fulani mbele yake.

Usikubali kupambana na watu juu ya maono yako , utapoteza maono , we pambana na maono yako toka kwa Mungu.

Daudi akukubali kupambana na Sauli mfalme , alimkwepa na kumpa heshima , ingawa alimfanyia mengi mabaya mno lakini hakuna mahali unaona akipanga nae vita.

Acha kupoteza Muda na wanadamu wenzio , kama Mungu amekupa maono hayo , kaa kimya muache mwenyewe ayatimize na kukuhinua lakini usijaribu kutumia mda wako kupambana na watu juu ya maono uliyopewa ,hiyo ni mbaya sana mtu wa Mungu ,muache Mungu mwenyewe afanye kitu alichokueleza , kaa kimya tu.

Neno linasema kuwa Daudi alizidi kuwa mkuu sana , maana Bwana alikuwa pamoja nae ,Mungu akiwa pamoja nawe ,hata wakupake mavi utang'aa tu.

Hata wachimbe kaburi na kukufukia ndani kwa uweza wa Yesu utatoka na utatembea tu na kila mtu atajua huyu ni mbarikiwa wa Bwana.*

Tambua jambo hili "Mungu kunyamaza mbele ya adaui zako, haimaanishi adui zako wameshinda".

Nikutie Moyo wakati unajiandaa kwenda kazini, Acha kupoteza mda na wanadamu , simamia maono yako.