March 25, 2018

Utambue umuhimu wa baba katika familia.

Kama kuna dhambi ambayo wanadamu wengi tutahukumiwa kwayo basi ni hii ya kumpuuza baba. Baba ni nguzo na kichwa cha familia anaepambana kwa nguvu zote kuhakikisha familia inakula, kunywa na kuvaa pamoja na mahitaji yote ya msingi ila kwa bahati mbaya watoto anaowalisha hadi wakakua wanaishia kusema tu nani kama mama. Hakika wababa wengi wamekufa bila kupewa shukrani stahiki na watoto wao. Baba anakuwa tayari kushinda njaa kazini ili hela aliyopata akanunue chakula ale na mke na watoto wake.

Wapo wababa wanaoungua jua kutwa nzima, wengine ni walinzi wanafanya kazi karibu masaa 24 ili tu kuhakikisha mke na watoto wanapata mahitaji ya msingi, kazi ngumu wanazofanya mda mwingi saa zingine huwafanya kuwa busy na kukosa hata muda wa kukaa na familia ila utasikia watoto wanasema baba hatupendi. Mchango wa baba ni mkubwa japo hauonekani kirahisi ila ukitaka kujua thamani ya Baba uliza tabu wanazopitia katika malezi wanawake wajane waliofiwa na waume zao
Tafadhali usipite bila kumpa neno la SHUKRANI na pongezi BABA yako kwa kukulea.