March 25, 2018

Visa 4 kati ya 10 vya saratani vinaweza kuepukika-Utafiti.

Utafiti mpya unaeleza kuwa karibu visa vinne vya saratani kati ya kumi vinaweza kuzuiwa kama watu wa nchi hiyo watabadili maisha yao kwa kupunguza kiwango cha kunywa pombe, kuacha uvutaji sigara, na vingine vinavyopelekea magonjwa ya saratani.

Utafiti huo ambao umefanywa na Cancer Research UK (CRUK) nchini Uingereza umeonesha kuwa zaidi ya kesi 2,500 zinazoripotiwa kila wiki zinaweza kuepukika kama watu wa nchini humo wataachana na lifestyle ya hatari hususani ya uvutaji sigara ambao huchukua zaidi ya 15% ya kesi zote za saratani.

Mwandishi Mkuu wa utafiti huo Dr Katrina Brown nusu ya wanaougua ugonjwa wa saratani ya mapafu ni wale wanaovuta sigara.