March 15, 2018

Wanandoa fanyeni haya mfurahie msisimko wa tendo la ndoa.

Tendo la ndoa linaleta maana kama wanaolitenda wote watalifurahia. Baada ya tendo, kila mmoja awe amekata kiu yake.

Kinyume chake, tendo linapoteza maana. Mmoja akiwa anainjoi na mwingine hainjoi, yule ambaye hainjoi hujikuta akiingia kwenye mawazo mazito.

Anatamani na yeye ainjoi kama mwenzake lakini bahati mbaya kila siku yeye anajikuta akiambulia maumivu.

Mhusika asiyeinjoi huwa anaegemea kwenye dhana mbili; kuna ambaye hainjoi ana uwezo wa kumwambia mwenzake kwamba hainjoi lakini kuna mwingine hawezi.

Anakuwa mzito kusema kwamba siinjoi. Badala yake anamueleza shosti au rafiki yake. Akikutana na rafiki mhuni, atamshauri achepuke ili aweze kuinjoi mapenzi.

Kama upo kwenye uhusiano na una dhana hiyo ya pili, unapaswa kubadilika. Jitahidi kumueleza mwenzako kwamba haufurahii tendo. Kwa kumwambia, mtapata suluhu ya pamoja na hakika mtainjoi.

Kwa msingi huo nilioanza nao, nalazimika leo kukueleza wewe msomaji wangu kwamba kuna mambo ya kufanya ili kuhakikisha mnalifurahia tendo tendo hilo na kila mmoja anaridhika.

MAANDALIZI: – Hili ni eneo muhimu sana ambalo wengi wetu huwa tunashindwa kulitendea haki. Wengi wetu tumekuwa tukikurupuka tu na kulifanya tendo.

Mwanaume amuandae mwanamke na mwanaume pia amuandae mwanamke. Muende sawa. Usiwe na papara ya kuparamia tu mwili wa mwenzi wako, wekeni muda mrefu wa kukusanya hisia zenu eneo la tukio.

TULIZA AKILI: – Tendo la ndoa ni muhimu sana ukalifanya ukiwa umetuliza akili. Mawazo yako yote yanapaswa kuwa eneo la tukio, akili yako iwaze uzuri na raha unayoipata kutoka kwa mwenzako.

Mara nyingi watu wengi hususan wanaume wamekuwa wakilifanya tendo hili huku akili

yao ikiwaza mambo mengine kama kukosa kipato, kukosa dili na kadhalika.

Matokeo yake hujikuta wakiwatesa wenzi wao ambao wanakuwa wameweka akili yote katika eneo la tukio. Mwanamke anafika safari yake, mwanaume akili haipo.

Anaendelea tu na safari bila kujua wakati huo mwenzake pengine alishachoka. Utayari naye wakati huo unakuwa haupo, hafurahii tena tendo, anaumia tu kutokana na shughuli inayoendelea.

Mnapotofautiana kifikra, tendo linapoteza mvuto. Halizai matokeo chanya kati ya wapendanao, ndio maana huwa kuna zile kauli za ‘fulani bwana huwa ananipatia’.

Kauli hizo ndizo ambazo zinasababisha mpasuko. Mtu analazimika kuisaka furaha nje ya mtu wake. Amani inatoweka na madhara makubwa hutokea likiwemo hata suala la kuachana.

USHIRIKIANO: – Wakati wa tendo, kila mmoja wenu anapaswa kutoa ushirikiano wa asilimia mia. Mwanaume unapaswa kujua sehemu muhimu ya mwenzi wako. Umguseguse kumpa hamasa au muwashawasha wa mahaba.

Mwanamke nawe vivyo hivyo. Ujue mwenzi wako akishikwa anakuwa taabani. Anafurahia tendo, mtasaidizana katika kufika safari yenu pamoja.

Wakati wa tendo, mwanaume usiwe bubu. Mwanamke anapoimba ‘nyimbo’ zake za furaha, unapaswa kumuonesha ushirikiano kwa kutoa sauti ya kuonesha kwamba unainjoi.

Toa sauti za kuonesha unapata burudani, itampa nguvu mwenzako ya kuongeza morali ya tendo. Msifie kwa maneno mazuri. Maneno kama ‘baby nainjoi, nakupenda, nafurahia kuwa na wewe’, yanaongeza ufanisi wa tendo.

Onesha kwamba unafurahia tendo. Hisia zako zote ziwe pale ili muweze kuweka utulivu wa tendo a mkienda sawa mtajikuta kwenye ulimwengu wenu wa raha ambao hamjapata kuusikia kabla