April 9, 2018

Faida za mti wa Mlonge kwa mama anayenyonyesha

Maziwa ya mama ndiyo yanakubalika na jamii kama chakula bora zaidi cha mtoto kwani  yana kinga ya mwili na viinilishe muhimu kwa ajili ya mtoto na yana kila kitu kinachohitajika katika kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi, aleji na kumpa mtoto kinga ya mwili na afya kwa ujumla.
Kuhusu Mti wa mlonge:-
Majani ya mti wa mlonge yana kiasi cha kutosha cha vitamini na madini matano mhimu zaidi kama madini ya chuma, kalsiamu, Vitamini A, E na K.

Mti wa mlonge una Madini chuma yanahitajika katika kuzuia uchovu .

Mara baada ya kujifungua mama wengi wanatokewa kuwa na upungufu wa madini ya chuma kama matokeo ya kupotea kwa damu nyingi wakati wa kujifungua jambo ambalo linaweza kupelekea hali ya uchovu sugu na udhaifu wa mwili kwa ujumla.

Kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa majani ya mlonge kina zaidi ya asilimia 46.8 cha mahitaji yako ya madini chuma kwa siku.

Matumizi ya mlonge kwa mama anayenyonyesha yatapelekea kumuondolea uchovu na kumuongezea kiasi kingi cha maziwa kwa ajili ya mtoto.

Mlonge una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach

Mti wa mlonge una Kalsiamu  ambayo ni mhimu katika kuimarisha mifupa na meno kwa wote mama na mtoto. Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Mlonge una Vitamini K husaidia damu isigande na ni mhimu hali hii kwa mama anayenyonyesha na kwa mtoto pia.

Vitamini K kwa kawaida hutolewa kwa watoto kwa njia ya sindano au vidonge mara tu wanapozaliwa. Ni vitamini mhimu kwa wamama ambao wanaweza kupatwa na tatizo la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.