April 1, 2018

Historia fupi ya maisha ya Aslay.

Isihaka Nassoro amezaliwa 6 Mei, 1995 ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania maarufu kama "Aslay". Alianza kufahamika kuanzia mwaka 2011 baada ya kutoa kibao chake cha Nakusemea alichokitoa akiwa chini ya Mkubwa Fella.

Baadaye akatoa nyimbo kadhaa kabla ya kuundwa rasmi bendi ya vijana ya Yamoto Band. Bendi ambayo ilidumu tangu 2013/2014 hadi 2017 ilipovunjika kwa sababu mbalimbali. Kuanzia 2017, Aslay akawa msanii wa kujitegemea bila bendi wala usimamizi wa Mkubwa Fella.

Amebaki na meneja wake wa zamani Chambuso. Akiwa msanii wa kujitegemea, ametoa nyimbo nyingi mfululizo hali ambayo imechanganya wengi, lakini mwenyewe alielezea kwanini amefanya hivyo, kwamba ni kwa sababu hana nyimbo nyingi alizofanya akiwa msanii wa kujitegemea zaidi ya zile alizokuwa na Yamoto Band.

Pia ili asiimbe za Yamoto akiwa kwenye matamasha, ndio sababu hasa ya kutoa nyimbo nyingi. Nyimbo hizo ni pamoja na Angekuona, Usiitie Doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo, Pusha Natamba na Huna. Awali ilitazamika kama Mkubwa Fella ndiye hasa mmiliki wa muziki wa kizazi kipya, lakini kupitia Aslay, Chambuso anasema si lazima yeye ndiye awe meneja bora wa muziki huu.

Source: Wikipidia