April 26, 2018

Jambo walilokanusha wataalamu kuhusu umri wa kujifungua.

Kumekua na mitazamo na taarifa mbalimbali kuhusiana na madhara mbalimbali yatokanayo na wanawake wenye umri mkubwa wanaposhika ujauzito kuweza kujifungua watoto wenye matatizo ya kiafya hususani utindio wa ubongo jambo ambalo Mkunga maarufu nchini England ameeleza sio sahihi na hata kama kuna hatari za jambo hilo sio kubwa kwa kiasi hicho.

Mkunga huyo Prof. Cathy Warwick ambaye ni Mkuu wa Chuo ch Wakunga nchini humo ameeleza kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na trend ya wanawake wengi kujifungua wakiwa na na umri wa kuanzia miaka 28 hadi 45 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za kiafya, mazingira, za kimasomo, kikazi na mengine jambo linalozua mijadala mingi ya kuwaibulia hofu wanawake wengi.

“Hata kama mwanamke atapata mtoto kati ya miaka 42 na 45 anaweza kupata mtoto asiye na matatizo kama tu mama huyo ana afya ya kutosha na hivyo watu waache kuogopesha wakinamama hawa.” – Prof. Warwick