April 13, 2018

Jinsi ya kufanya mbwa wako yeyote awe mkali.

Umeshasikia watu wakikushauri umlishe wako bangi?unga wa risasi? au Nyuki?
Sahau kuhusu hivyo vitu kwa sababu sio tu kwamba havisaidii bali ni haramu na vinaweza kumuua mbwa wako!

Leo nitakufundisha njia ambazo unaweza kumfanya mbwa wako awe mkali maisha yake yote.

Kwanza unatakiwa uelewekwenye mbwa wa ulinzi kuna vitengo vingi vya mbwa. mfano

1. Mbwa mwangalizi(Watch-dog)
- hawa mbwa mara nyingi hawang'ati mtu,ila wanabweka sana, wako makini sana kuangalia usalama wa eneo wanaloishi na kama kuna kishindo,sauti au kitu chochote kimeingia eneo lake lazima apike kelele kwa kubweka, wanasaidia sana kukujulisha kama kuna mtu ameingia bila ruhusa nk

2. Mbwa wa mashabulizi.
-mbwa hawa wanatumia kwa ajili ya kushabulia kwa kung'ata, sio lazima wabweke kabla ya kung'ata na wanaweza kung'ata bila taarifa. Wanatumika na polisi na jeshi na hata mtu binafsi anaweza akawa nao. wakifundishwa vizuri wanaweza kumweka chini na kumjeruhi mtu mzima mwenye silaha mara nyingine hata zaidi ya mtu mmoja. na kwa jeshi la marekani wananunua mbwa wa mashabulizi alifundishwa kwa kiwango cha juu kwa dola za kimarekani zaidi la 50,000(Zaidi ya milioni mia moja za kitanzania).
Ubaya wa mbwa hawa ni kwamba wanaweza kuleta madhara makubwa na kusababisha kesi hadi ya mauaji.

Viko vitengo vingine ya mbwa kama mbwa wa kuwindia, mbwa wa kuhudumia, na mbwa wa uokoaji na utafutaji, ila kwa leo tutaongelea mbwa wako wa ulinzi.

NJIA ZA MUMFANYA MBWA WAKO AWE MKALI.
Kwanza unatakiwa ujue unataka mbwa wako awe wa nini! 1. awe wa kubweka na kukushtua pale tukio linapotokea mfano mwizi kaingia 2. au awe anaenda moja kwa moja kwenye kushambulia 3. Awe na sifa zote?

Ili kummfanya mbwa wako awe mkali unatakiwa uelewe saikolojia na sosholojia ya mbwa wote.

Mbwa yeyote ni mlinzi mzuri na anaweza kuwa mkali, makosa yanafanywa na mfugaji siku zote na sio mbwa.

ELEWA KIDOGO KUHUSU MBWA, ITASAIDIA JINSI UTAKAVYOWAFUNZA MBWA WAKO.
Mbwa ni wanyama wa kujamii(Social Animals)na wenye uelewa mkubwa sana. Wanaishi katika jamii ambayo inayoongozwa na mbwa mwenye nguvu kuliko wote. Jamii wanayoishi inaitwa PACK.
Kwenye jamii kila mbwa ana cheo chake na kiongozi wa PACK anaitwa ALPHA wakati wenye cheo cha kati wanaitwa BETA na wasio na cheo kabisa wanaitwa OMEGA.
Mfumo wa nidhamu ambao mbwa wamejiwekea ni kwamba mwenye cheo cha juu(ALPHA) lazima ale wa kwanza kabla kabla ya wengine(BETA na OMEGA). Baada ya kushiba atafuata BETA kisha OMEGA. Atakayeharibu utaratibu ataambulia kipigo bila ya huruma kutoka kwa mbwa mwenye cheo cha juu yake.

Kumbuka mbwa wanapigana kila siku na sababu kubwa ni kutaka kupanda cheo- KUMPINDUA ALPHA, au Omega KUMPINDUA Beta au kuonyesha utawala wake sio wa mashaka.

Mbwa hawajui kutofautisha mtu na mbwa ki hadhi, kwa hiyo wanachukulia mtu anayewafuga kama mmoja wao na mara nyingi wanachukulia kama ALPHA, na pale anapokuona hufai kuwa kiongozi wake atajaribu kukupindua ili yeye awe APLHA na wewe uwe chini yake.
Kama mbwa wako hakueshimu, na anakuonyesha ukali ujue ameshakupindua, na anataka ufanye anachotaka yeye.

SABABU ZINAZOMFANYA MBWA AWE MKALI.

Mbwa yeyote anakua mkali kwa sababu moja au baadhi ya sababu zifuatazo.

1. Ana stress
2. Anaumwa au Maumivu.
3.Analinda cheo chake.
4.Analinda usalama wa PACK, kama vile kumlinda anayemfuga, kulinda watoto wake, kulinda mali au kitu chochote kilicho eneo lake(mali ya pack)

Hii ndio sababu mbwa aliyefungwa anakuwa mkali- kwa sababu ya kuwa na stress nyingi kutokana na kukosa uhuru wa kufanya anachotaka.

Watu wengi wanafanya makosa ya kuwapa mbwa unga wa risasi ambao unakatakata utumbo wa mbwa na kumfanya awe na hasira. Unaweza ukajaribu kufikiria hasira ambazo ungekuwa nazo kwama unaumwa na tumbo alafu watu wanakuchezea!!!

Ningependa kuonya kuhusu kumlisha mbwa wako bangi, kumwekea nyuki, au unga wa risasi, Hivyo vyote havimfanyi mbwa wako apende kulinda PACK, zaidi ya yote vinamfanya kuonesha hasira kutokana na maumivu anayopata.

Unga wa risasi unaweza kumwua mbwa wako pia, na hasira anazokuwa nazo hazitakua kwa mgeni au mwizi tu, bali hata kwako, watoto wako,watu aliowazoea, mifugo nk.

Achana na hivyo vitu kabisa!!! Heri kutumia njia ya stress ambayo nitakufundisha jinsi ya kuifanya.

1. NJIA YA KUMPA MBWA WAKO STRESS
Hii ni njia rahisi sana ambayo watu wengi wanaitumia ila hawajui inafanyaje kazi, namna ya kufanya sahihi, na jinsi gani ya uiboreshe ili ifanye kazi vizuri zaidi. Kama ukiitumia vizuri itamfanya mbwa wako awe mkali, aweze kufanya mashabulizi na pia abweke kukujuza kuhusu hatari iliyopo.

Hii ni njia ya kumfunga mbwa kwenye banda au mnyororo mbali na macho ya watu.

JINSI YA KUITUMIA VIZURI NJIA HII.
Kwanza unatakiwa kuondoa hofu na uoga wa asili kwa mbwa wako. Kumbuka kiumbe chochote kina hofu, ila hutapenda mbwa wako aoneshe hofu kwa mwizi, au sio?

Hii mbinu unatakiwa uanze mbwa akiwa mdogo kwazia siku ya Kwanza kuzaliwa hadi afike umri wa miezi 3 hadi mitatu na nusu.

Kipindi hiki usimfunge sana mbwa wako, muache amzoee kila mtu wa familia, mwache acheze na kujifunza vitu mbalimbali, mfundishe jina, mfundishe kuwa na adabu na kikubwa cha muhimu USIMPIGE MBWA WAKO AKIWA MDOGO - utamfanye akuwe akiwa mwoga, Mwizi anashika fimbo mbwa aanze kupiga ukunga, au akiona jiwe anakimbilia kwa jirani.
Kama akikosea akiwa na mwezi 1 na kuendelea, ndani ya sekunde 5 za kufanya makosa unatakiwa umshike nyuma ya shingo na onyesha sura ya ukali na umpiga vibao polepole kwenye mashavu(Kama ana mashavu. Hahahaha!) huku ukimfundisha neno utakalokuwa ukimwambia akiwa anafanya makosa.

Mfano akinya ndani unampelepa hadi alipokunya, unamshika ngozi ya nyuma ya shingo unamwonyesha mavi yake huku unampiga vibao taratibu ila asikie maumivu, usiache kutumia neno mfano ACHA kila unapopiga kofi. Akiwa mkubwa sio lazima kumpiga ukisema ACHA atajua hupendi ilichofaya au anachofanya. Kutumia fimbo na mawe kwa mbwa wako akiwa mdogo kutamjengea uoga wa hivyo vitu akiwa mkubwa.

KUMBUKA SIKU ZOTE WEWE KUWA APLHA KWA MBWA WAKO.
Ni lazima umtembeze eneo lenye watu tofauti ili aondoe uoga wa watu, na nilazima umzoeshe kelele mbalimbali ili azizoee akiwa mdogo, kama kishido, kelele za mabati nk, hutafurahi mwizi akikanyaga bati mbwa aingie chini ya banda!!!Anatakiwa azoee akiwa mdogo, ajue kelele na watu hawana madhara yoyoye kwake na hiyo inamwandaa kuja kuwa mlinzi asiyeogopa mtu yeyote.

Lazima umwache acheze vya kutosha, unaweza kucheza naye pia ambayo itafanya urafiki wenu uwe mkubwa zaidi na ajaribu kukulinda kila anapoona uko kwenye matatizo mfano Unapigana!
Lazima uwe unatembea naye kwenye mipaka ya nyumba yako, akiwa mkubwa hataruhusu mtu au kitu kuvuka hiyo mipata. Ndo mana wanasema mbwa mkali kwao!!!

KAFIKISHA MIEZI MITATU
Hapa ndio anaanza safari yake ya kuja kuwa mlinzi, na hapa ndio unatakiwa kumtenga kabisa na macho ya watu, Itabidi aishi kwenye banda au mnyororo kwa masaa mengi na asimwone mtu yeyote, Unamfungua usiku amao unajua hakuna watu wa kuonana naye zaidi yako na wana familia.

KUFUPISHA.
Kumfunga wakati amezoea kuwa huru kutamfanya apate stress, atapiga kelele mara ya kwanza na akiona hawezi kutoka atatulia. Ila uchungu alio nao atakuja kuonyesha kwa kumtolea uvivu mwizi.
Kumbuka mbwa karibu wote wanaonyesha ukali sana wakikaribia na baada ya kutimiza mwaka mmoja. Hii inawafanya wawe wamebalehe na homoni zinawafanya wawe wakorofi,wene hasira na wakali