April 26, 2018

Mambo 5 ya kuzingatia ili kumpata mtoto wa kike.

Kwa wakati mwingi, mwanadamu haridhiki na mambo mengi. Ukitazama, wazazi wengi hupenda kupata watoto wa kiume lakini badala ya wa kiume hupata wa kike au akitaka wa kike anapata wa kiume

Kama ungetaka kumpata binti, hizi ndizo mbinu 5 utakazotumia

1. Mbinu ya Shettle
Njia hii imekuwa ikitumika kuanzia miaka ya 1960 iliyoanzishwa na daktari Shettles. Jambo muhimu katika mbinu hii ni kujua muda wa siku zako za hedhi. Hivyo, utajua siku za yai kuachiliwa. Kwa mbinu hii ya Shettle, unafaa kufanya mapenzi kati ya siku mbili au nne, kabla ya kuachiliwa kwa yai.

Mbegu za mtoto wa kike zinazotoka kwa mwananume huwa nzito na hivyo huenda polepole kuliko mbegu za kiume. Mbegu za kiume hukimbia haraka na hivyo zitaweza kufa hata kabla kukutana na yai.

Usifanye mapenzi ukiona 'kamasi' nyeupe kwani hii inaonyesha kuwa yai linaachiliwa, la sivyo utapata wa kiume kwani mbegu za kiume hukimbia haraka sana.

2. Namna ya kukaa ukifanya mapenzi (Style)
Kama unataka kumpata mtoto wa kike, tafuta "style" ambayo mwanaume hataingia ndani sana wakati mnafanya mapenzi.

Mtindo wa "Kimishonari" ndio hupunguza uwezekano wa mwanaume kuingia ndani sana.

3. Usifike upeo mapema
Wakati mnafanya mapenzi, hakikisha haufikii upeo wa mapenzi mapema kuliko mumeo kama unataka mtoto wa kike. Hii ni kwa sababu mwanamke akifika upeo huachilia maji ambayo hufanya mbegu za kiume kuishi kwa muda mrefu.

Hivyo, maji hayo yakikosa, mbegu za kiume zinaweza fariki na kuipa ya kike nafasi.

4. Kula vyakula vyenye chembe za asidi
Mambo 5 ya kuzingatia ili kumpata mtoto wa kike
Kwa kawaida, mbegu za kiume hufa haraka katika mazingira yenye asidi. Japo si vizuri mwili kuwa na kiwango cha juu cha asidi, kula vyakula vyenye asidi kwa wakati huo ili kupata mtoto wa kike

5. Punguza matumizi ya chumvi
Unaweza punguza chumvi katika vyakula kama vile nyama kati ya vyakula vingine. Viwango vya chini vya chumvi humpa mwanamke nafasi kupata mtoto wa kike.

Source: Wikihow