April 1, 2018

Millard Ayo, mtangazaji tajiri zaidi Tanzania, analipwa Mil 50-80/month.

Kwanza kabisa nikupe hongera Millard ayo kwa kazi nzuri unayofanya ya uandishi wa Habari. Wewe una kipaji kikubwa sana.

Presenter millard Ayo ndio anayetajwa kuwa mtu anayepokea royalities za Youtube nyingi zaidi baada ya Diamond Platnumz katika nchi ya Tanzania, hii ni kutokana na viewers na subscribers wa channel zake ambapo kwa mwezi malipo yake huwa yana range mil 50 hadi 80 kutokana na idadi ya viewers, diamond anarange 80mil-130mil kwa mwezi.

Kwakweli nimpe hongera kwani ameajiri vijana wengi (zaidi ya 10) ktk online TV yake.
Vijana nawaasa muwe wabunifu kama millard na mtafanikiwa sana. Millard ayo tunatarajia kuona mambo zsidi kutoka kwako, ikiwezekana ufungue kituo cha radio na television kwani una mashabiki wengi.

Wengine wanaovuna mkwanja mkubwa you tube ni Global tv, Harmonize, Rayvanny. Actually hata wasanii ambao sijawataja nao wanapata pesa nyingi tu.