April 8, 2018

Sababu zinazopelekea wazee wengi kupatwa na matatizo ya akili na upungufu wa kumbukumbu.

Inawezekana umewahi kusikia watu wakisema kwamba mtu akifikia umri fulani ubongo huacha kukua basi wataalamu wamekuja na utafiti mpya ambao unapingana na tafiti hizo za zamani.

Ilikuwa ikiaminika kupitia tafiti za zamani kuwa ubongo huweka kitua katika ukuaji jambo linalopelekea wazee kuwa waathirika wakubwa wa magonjwa ya akili.

Hatahivyo Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, New York wamegundua kuwa maelfu ya seli mpya za ubongo hutengenezwa muda wote mtu akiwa mzee.

Hivyo hii inamaanisha kuwa matatizo ya akili au upungufu wa kumbukumbu kwa wazee hayasababishwi na upotevu wa neurons bali seli za ubongo kushindwa kuwasiliana ipasavyo.