April 6, 2018

Tiba asili za kuondoa michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi yako.

Kula Lishe Bora

Kama tulivosoma pale juu kuna uhusiano mkubwa kati ya uzito mkubwa na kitambi na kupata mikunjokunjo. Hivo punguza vyakula vya wanga na sukari na kula zaidi vyakula vya mafuta kama nyama, parachichi, nazi namafuta ya nazi, samaki nk. weka ratiba ya kupunguza unene wako uliopitiliza kwa kufanya mazoezi na kushugulisha mwili wako. baadhi ya vyakula vingine  vya kutumia kwa wingi kwenye safari yako ya kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi ni kama
Mbegu za maboga: mbegu za maboga ni muhimu sana kwa afya ya ngozi husaidia katika kurekebisha homoni ya estrogen na kuongeza uzalishaji wa collagen. unaweza kutafuna mbegu zake pekee ama ukasaga unga ukatumia kama chai ama kweye uji.

Vyakula vyenye majimaji: mwili unapokosa maji hupelekea tumbo kuwa kubwa kwa kujaa gesi. vyakula hivi ni kama matikiti maji, papai, machungwa na matango

Vyakula vyenye kambakamba: hii inajumuisha mbogamboga, karanga, mbegu na zabibu. Vyakula vyenye kambakamba/fibers zina viondoa sumu (antioxidant) kwa wingi sana vitakusaidia kusafisha ngozi na hivo kuzuia kuzeeka haraka kwa ngozi.

Protini kutoka kwenye vyanzo halisi mfano kutoka kwa wanyama waliokuzwa kwa kula nyasi (grass fed beef), mayai ya kinyeji, na virutubisho vya protein mfano Green world Protein powder inaweza kukusaidia mahitaji yako ya kila siku ya protini kwa upande mwingine punguza ama epuka vyakula kama:- vyakula vilivyosindikwa na kusafishwa sana ikiwemo unga na nafaka: vyakula hivi vinapochakatwa na mwili hubadilishwa kuwa sukari na kisha kuhifadhiwa kama mafuta kwenye makalio,na chini ya ngozi.

Sukari: Sukari husababisha ukuaji wa bateria wabaya kwenye mfumo wa chakula, na hivo kuzorotesha kinga yako ya mwili, kinga inapokuwa chini huongeza hatari ya mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula, na kisha kuleta aleji ya vyakula.

Vyakula vya ngano: vyakula vya ngano vina portini ngumu ndani yake inayoitwa glutein. protini hii huleta ugumu wa kuchakatwa kwenye mfumo wa chakula na hivo kusababisha mcharuko na aleji. Mcharuko huu huleta matokeo mabaya kwenye ngozi kwa kuathiri usafirishaji na kupunguza uwezo wa mwili kufyonza virutubishi.

Tumia Collagen ya Kutosha

Kama tulivojifunza mwanzoni ni kwamba Tishu za ngozi zimetengenezwa kwa protini za Collagen. Kwahiyo kama ngozi yako ipo imara basi utapunguza uwezekano wakupata mikunjokunjo. Collagen ni protini inayopatikana kwa wingi kwenye ngozi na husaidia kuvutika na kufanya ngozi kuwa hai na laini. Chanzo kizuri cha Collagen ni kunywa supu ya mifupa (bone broth) . Supu ya mifupa ina amino acid kwa wingi ambazo hutengeneza collagen. Collagen iliyopo kwenye Supu ya mifupa  husaidia kuimarisha tishu za ngozi na kuondoa tatizo la cellulite.

Tumia virutubisho

Vya kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi na michirizi (anti-cellulite Suppliments): unaweza kufika ofsini kwetu ukatumia virutubisho kama Royal gel na sipiriluna vikakusaidia kupambana na tatizo lako bila kikwazo.

Fanya mazoezi kila mara

Mazoezi ni njia nzuri sana pale unapotaka kupunguza uzito, tumeona pale juu athari za uzito mkubwa na kitambi kwenye kupata mikunjokunjo, pamoja na kula lishe nzuri ni muhimu sasa uweke ratiba ya kufanya mazoezi walau mara tatu kwa week.

Tumia mafuta asili ya nazi kwenye kutibu ngozi yako.

unaweza kutumia mafuta halisi ya nazi kwa kupaka kwenye ngozi yako baada ya kuoga. Kumbuka cream za madukani zinaweza kuwa ghali na hatari kwa afya yako kwa maana zina kemikali na metali nzito ambazo ni sumu kwa afya ya ngozi.