April 1, 2018

Wanasayansi wakuta amri kumi za Mungu katika sayari ya Mirihi (Mars)!!

WANASAYANSI WAKUTA MAANDISHI YA AMRI ZA MUNGU KATIKA SAYANSI YA MARS
Moja kati ya mitandao maarufu Dailry Current, ambao ni mtandao wa habari za hapa na pale nchini marekani uliandika makala hii juu ya "Wanasayansi wakuta amri kumi za Mungu katika sayari ya Mirihi (Mars)" lakini watu wengi wamepinga na kusema ni uzushi, hakuna kitu kama hicho. 

Kabla ya kusoma makala hii nataka ujiulize Je ni kweli wanasayansi wamewahi kufika Mars? Na baada ya kusoma makala hii usisahau kucomment mawazo yako pia hapo chini.

Linapokuja swala utandawazi kila mtu anaweza kuandika na kutangaza chochote kile kwa wakati wowote ule na kikasambaa kuifikia dunia nzima, iwe ni kweli ama ni uongo. Binafsi siamini kwamba habari hii ni habari ya kweli, nadhani mtandao uliochapisha habari hii ulikuwa unatafuta kiki tu katika masikioa ya wanamitandao.

Hivi ndivyo mtandao huo ulivyo andika juu ya story hiyo:-

"Wanasayansi wa anga za juu wa kampuni ya NASA ya Marekani wameshangazwa na kukuta maandiko ya amri kumi za Mungu na andiko la Yohana 3:16. (Yohana 3:16 BIBLIA inasema ''kwa maana jinsi MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.) 


Wanasayansi hao waliingia kwenye pango moja kujalibu kutafuta maji na  kukuta maandiko hayo kwenye pango katika sayari ya Mars yakiwa yameandikwa kwenye mawe.

Maandishi hayo yaliyoandikwa kawa  lugha 7 tofauti nazo ni English, Spanish, Chinese, Basque Hebrew na lugha yingine hazikutambulika.

Wanasayansi hao wameshangwazwa na jambo hilo na kuwafanya wao waamini kuwa ni dini ya kikristo tu ndiyo ndini ya kweli kutoka kwa Mungu.

Kati ya wanasayansi hao ambaye yeye ni muaustralia na anafanya kazi NASA ambao wako huko tangu Agosti mwaka jana, wameshangaa maandiko hayo yamefikaje huko zaidi ya kuona kuwa kweli MUNGU yupo,


Wanasayansi hao wako huko kuchunguza sayari hiyo ili kuona kama kuna uwezekano wa binadamu kuishi huko jambo mpaka sasa inasemakana kuna uwezekano wa viumbe hai kuishi kuko kutokana na vitu vingi kushabihiana na huku Duniani."


Je habari hii ni kweli ama iliandikwa siku ya sikukuu ya wajinga!