April 1, 2018

Wasifu mfupi wa mbunge singida mashariki Tundu Lissu.

Jina kamili ni Tundu Antipas Mughwai Lissu. Alizaliwa Januari 20 mwaka 1968 mkoani Singida nchini Tanzania. Kwa sasa ana umri wa miaka 49.


Mawasiliano.
Simu: +255 22 2780859
+255 754 447323
+255 786 572 571
S.L. P. 21746, Dar Es Salaam
Barua pepe: tlissu@parliament.go.tz

Elimu:
1995 – 1996 – Chuo Kikuu cha Warwick Uingereza, Shahada ya umahiri ya Sheria,
1991 – 1994 – Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
1987 – 1989 – Shule ya Sekondari Galanos mkoani Tanga, kidato cha tano na sita.
1983 – 1986 – Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Kilimanjaro
1976 – 1982 – Shule ya Msingi Mahambe mkoani Singida.

Kazi:
1990 – 1991 – Mwalimu katika Shule ya Sekondari Bondeni, Arusha,
1995 – 1997 – Mwanasheria wa kampuni ya D’Souza Chamber,
1999 – 2002 – Mtafiti katika taasisi ya ‘The World Resources Institute’ (WRI),
2002 – 2009 – Mtafiti katika taasisi ya ‘Lawyers’ Environmental Action Team’ (LEAT),
2004- hadi sasa- Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
2017 – Raisi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Siasa.
Tundu Lissu ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na amekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kuanzia mwaka 2010 hadi sasa ambapo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 aliweza kutetea kiti hicho.
Mwaka 1992 – 1996, Tundu Lissu alikuwa mwanachama wa NCCR Mageuzi na mwaka 1995 aligombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Maisha Binafsi.
Tundu Lissu ameoa na mke wake anafahamika kwa jina la Alice Lissu.