May 30, 2018

Dalili 7 za mwenza kuwa na mchepuko au kukusaliti

Leo naomba pia niongelee kuhusu dalili ambazo zinaweza konekana kwa mwenza wako ambazo zinapelekea kujenga fikra kwamba "unasalitiwa" dalili hizo ni kama zifuatazo:-

1. Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana)
Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae! Anakutumia tu huyo!

2. Sisi ni Marafiki tu!
Kwa ambao bado hawajaoana ukimuuliza mpenzi wako unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.

Kwa ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu!

3. Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu!
Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi wako na ndio maana anakuwa hivyo! Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani!

4. Mabadiliko ya Ratiba za Kazi
Kwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na dharula za kikazi zisizoisha mara vikao mara n.k!

5. Kutumia Muda Mwingi katika Computer
Kama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi za ofisini anamalizia!

6. Simu za Siri, Simu kuwa locked !
Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa au inawekwa silent!

Pia mambo ya kulock simu na hizi SmartPhone sasa mtu akishatupia kitu cha Pattern/Password/PIN ndo basi tena unatakiwa kuwa mjanja sana kuweza kumkamata.!

7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka!
Waswazi wanasema "Wasiwasi ndo Akili" Basi wasiwasi wako huenda ukakupa akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli!

Ukiyaona haya au ya kufanana na haya kaa ukijua kuna kidudumtu kinawala na kitawatenganisha, Ni vyema ukachukua hatua! Pia Jiandae Kudanganywa! As some people says kuwa love is a game so get ready kuplay na sio kuplay na kuwa loser but to be a winner.