May 7, 2018

Fahamu aina ya wanawake ambao wanaume upenda kuwa nao kimahusiano.

Kwa mwanaume mwenye malengo na msimamo na mahusiano yake mara nyingi uchagua ni nani wa kuwa nae katika mahusiano, hata kama atakosa vigezo vyote ila vipo ambavyo anaweza kuvizingatia kwa ukaribu zaidi.Hizi  baadhi ya sifa wanaume wengi upenda wanawake wao kuwa nazo.

1.Wenye msimamo.
Wanawake hawa mara nyingi huwa ni wa daraja la kwanza kwa wanaume, mwanaume anapenda mwanamke mwenye uelewa mkubwa na mwenye maamuzi yenye kuwa na msiamamo.sifa hii umfanya mwanaume amshirikishe mwanamke wake katika mambo mengi hata yale ya siri.

2.Wapenda usawa
Wanaume pia utaka mwanamke mwenye kupenda usawa wa jinsia, mtu anaeweza kubeba majukumu sawa na mwanaume n akuweza kusaidia.sio kila jukumu likitokea basi linakuwa linaegemea upande mmoja.

3.Marafiki.
Wanawake marafiki ni wale ambao wanakuwa karibu na wapenzi wao katika shida na raha, ni wale wenye kujua matatizo ya watu wao wa karibu na kutaka kuyabeba kuwa kama ya kwao pia.

4.Anaejua mapenzi.
Hii inakuwa ni moja ya mambo yanayoweza kumfanya mwanamke na mwanaume kuachana kwa urahisi pia, wanaume wanapenda wanawake walioo wajuzi na mafundi katika swala la faragha.Mwanamke anaejua jinsi ya kuondoa kiu ya mpenzi wake hudumu katika mahusiano.

5.Wapenda uwazi
wanawake wanapokuwa wenye kuongea na kusema kila jambo baya au uzuri pia inakuwa ni rahisi kufanya mahusiano kuwa yenye amani, mwanamke inabidi awe muelewa wa mambo , mkweli na awe msemaji wa vile vile anaona haviendi sawa katika mapenzi ingawa wanawake wengi hapa ukosea na kuwa waongeaji sana na kulalamika badala ya kuongea vitu vyenye msimamo.

6.Wanaojitegemea
Imezuka tabia kwa wanawake kuwa mwanaume ndio anatakiwa amuhudumie mwanamke kwa kila kitu, hii inawachosha wanaume kwa sababu na wao pia wana vitu wanataka kufanya tofauti na yale ya kwako.Mwanamke anatakiwa ajitegemee ila inapotokea kunahitaji msaada basi itaonekana na mtaweza kusaidiana  kama wapenzi.

7.Maridadi

Hakuna mwanamke anaevutia kama yule maridadi, msafi mwenye kujipenda na kujiremba pia.mwanamke anaekwenda na wakati tena mwenye kujali anavaa nini na wapi na kwa muda gani.Mwanamke anapaswa kuwa msafi ili kila napokutana na mwenzi wake , mwenzi wake anakuwa mwenye amani ya kuwa nae karibu.Mfanye mwanaume wako akusifie kila siku kila wakati.