May 15, 2018

Fangasi ukeni husababishwa na nini? Je kuna tiba ya fangasi?

CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenyengozi pia.

Bacteria hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, MFANO mabadiliko katika Hali ya PH tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0_4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali pia kupungua kwa Kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalmbali huletekeza kukua kwa Candida, ndio maana wagonjwa wenye maradhi ya UKIMWI na KANSA, ama wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kuumwa fangasi ya Candida. Candida pia hupatikana kwenye mdomo, tumbo, kwenye kwapa.

Hivo pale inapotokea fangasi hawa wa Candida kuanza kukua kupita kiasi bila kudhibitiwa kitendo hicho huitwa Candidiasis ama Yeast infection. Matokeo yake ni mfululizo wa maambukizi na kuumwa kwa mwili.

Bahati mbaya ni kwamba taarifa nyingi za mtandaoni zimekuwa zikipotosha pasipo kueleza kwa ufasaha juu ya tatizo hili na hivo kufanya uelewaji wa tatzo kuwa mgumu. hivo kama unasumbuliwa na tatizo hili na unapenda kujifunza na unahitaji kujua kuhusu dawa asili ya fangasi sugu basi endelea kusoma makala hii kwa umakini mpaka mwisho.

Ni muhimu kuelewa kwamba kukua kupita kasi kwa Candida siyo kwasababu Candida wanapatikana kwenye eneo husika, Hapana na ndio maana tatizo linakuwa gumu kutibika kutokanana na kwamba dawa nyingi huua Candida wote na kuua bacteria wazuri na hivo kuharibu msawazo wa mwili. Kumbuka uwepo wa Candida ni muhimu kwa ufanisi wa mwili.