May 1, 2018

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula au kunywa sumu.

Umewahi kusikia mtu amekufa kutokana na kula au kunywa sumu? Unajua ni kwa namna gani unaweza kutoa huduma ya kwanza ili kuokoa maisha ya mtu aliyepitia hali hiyo?

Mtandao wa first aid fir life unakuletea dondoo mbalimbali unazotakiwa kuzifuata ili kumsaidia mtu aliyekunywa au kulishwa sumu. Kwa mujibu wa mtandao huo, mifano ya sumu ni pamoja na dawa za usingizi, za kula wadudu, kemikali za viwandani pamoja na aina nyingine za dawa na kemikali ambazo hazifai kwa binadamu.

 Mtu akila sumu anahitaji kufanyiwa huduma ya kwamnza haraka ili kupunguza athari ambazo zinaweza kujitokeza. Sumu inayoingia tumboni inaweza ikapunguzwa nguvu kwa kunywa maziwa au maji mengi.

Dalili ya mtu aliyekula au kulishwa sumu Anaweza kupoteza fahamu, akashindwa kupumua vizuri, maumivu ya tumbo au kifua na kutapika au kujisikia kichefuchefu.

Jinsi ya kumsaidia Hatua ya kwanza, mgonjwa anatakiwa kuwekwa kwenye eneo lenye hewa safi au upepo wa kutosha ikishindikana hilo, apepewe. Inashauriwa mgonjwa ambaye bado ana fahamu zake asipewe kitu chochote cha kunywa hadi daktari atakapotoa maelekezo.

Kwa mgonjwa aliyepoteza fahamu apewe maji au maziwa kidogo kwa lengo la kumtapisha sumu iliyoingia tumboni. Endapo mgonjwa atapewa maji au maziwa na asitapike, unaweza kumsaidia kwa kumtekenya tekenya kwa vidole nyuma ya shingo yake au kooni ili aweze kutapika.

Wakati ukifanya hayo, andaa utaratibu wa kumpeleka hospitali au kwenye zahanati kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi. Ni muhimu pia kufahamu aina ya sumu ambayo amekunywa ili kumrahisishia daktari kujua anamsaidiaje mara ukimfikisha hospitali.