May 2, 2018

jinsi ya kupika keki. (Hatua nyepesi)

MAHITAJI:
-Mayai sita
-Siagi
-Sukari (icing sugar)
-Baking powder
-Unga wa ngano
-Mafuta ya kupikia
-Flavours za vanilla, chocu late au matunda

NAMNA YA KUANDAA
Chukua mayai yako sita (kwa keki ya ukubwa wa wastani), yagonge kisha chukua siagi (robo kilo) na uiweke kwenye bakuli, ongeza na sukari kwenye siagi kisha mimina mayai kwenye mchanganyiko huo. Koroga mpaka upate uji mzito, unaweza kutumia mashine maalum ya kuchanganyia.

Ukishapata uji mzito lakini laini, changanya na unga wa ngano, ongeza baking powder kijiko cha chai kisha weka flavour yoyote unayotaka keki yako iwe, inaweza kuwa vanilla, rose, machungwa, mananasi n.k.

Changanya mchanganyiko huo kwa kutumia mwiko kwa dakika mbili mfululizo. Chukua sufuria, ipake mafuta kwa ndani kisha chukua karatasi plain na kuiweka ndani ya sufuria. Mwagia mchanganyiko wako kisha weka kwenye oven na baada ya muda utaanza kusikia harufu nzuri.

Ukitaka kujua kama keki yako imeiva, chukua kijiti kikavu na kukiingiza katikati ya keki, kikitoka kikavu basi ujue keki yako imeiva, itoe na iache ipoe, unaweza kuongeza na mapambo unayoyataka, kama kuandika jina au kuweka rangi.