May 2, 2018

Jinsi ya kutengeneza uso na ngozi yako iwe soft kama ya mtoto mchanga.

Habari ya leo tena ndugu, ni matumaini yangu siku yako imekuwa njema sana leo!!!

Je unataka kuwa na ngozi nyeupe? ili iweje?. Wakati mwingine nakutana na wadada au wamama wamejichubua ngozi zao kutoka kwenye ueusi na kuwa nyeupe! nashangaa zaidi unakuta dada mwingine ni mweupe wa kuzaliwa kabisa lakini bado anapakaa madudu ya dukani eti ili awe mweupe zaidi!!

Hivi nini huwa ndiyo sababu kwa watu wenye tabia hizi? kwanini hamjiamini?

Haya ili kuwa na ngozi nyeupe kwa njia za asili na bila gharama yeyote na bila kukuachia madhara yoyote fuatilia dawa ifuatayo ya asili. Hii hasa haikufanyi uwe mweupe kabisa bali unaisafisha ngozi yako vizuri ili iwe na afya ile inastahili na kama imeaanza kufubaa basi itarudi kuwa na rangi yake ya asili na yenye kupendeza.

Ifanye Ngozi Yako kuwa nyeupe bila mkorogo

Hatua za kufuata:

Mahitaji:
    Asali kijiko kimoja cha chai
    Juisi (maji maji ya limau) kijiko kimoja cha chakula
    Maji ya uvuguvugu kiasi

Jinsi ya kutengeneza mchanganyiko wako
1. Changanya juisi ya limau na asali katika chombo kimoja kisafi na uchanganye ukitumia uma au kijiko cha kawaida kwa dakika kadhaa.

Matumizi
1. Osha uso vizuri ukitumia sabuni (kama unapata sabuni ya habbat soda inakuwa vizuri zaidi) na maji ya uvuguvugu kisha jifute na kitambaa kisafi
2. Jipake ule mchanganyiko wako usoni na maeneo yote ya shingoni taratibu huku ukijimasaji hivi kwa dakika 10
3. Osha uso kwa maji safi, mwisho jifute kwa taulo safi

Mhimu: Fanya zoezi hili kwa wiki mara 1 mpaka mara 3 na matokeo yake utaniletea hapa hapa