May 11, 2018

Mapenzi ni nini? Panua ufahamu wako juu ya mapenzi.

Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.

Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu ("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia.

Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usioelekea kabisa ngono na hata umoja wa kina au ibada ya upendo wa kidini.

Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa.

Mapenzi yasiyohusishwa na mtu maalum
Mtu anaweza kusema anapenda nchi, kanuni au shabaha maalumu ikiwa anaithamini sana na kuizingatia kwa makini.

Vilevile, katika huduma za huruma na kazi za kujitolea "upendo" wa kazi unaweza kutokana na mapenzi yasiyohusishwa na kitu pamoja na utu na imani za kisiasa badala ya mapenzi kati ya watu.

Watu pia wanaweza "kupenda" vitu, wanyama, au shughuli ikiwa wao wenyewe watajitolea kujihusisha na vitu vile. Ikiwa tamaa ya kingono pia inashirikishwa, hali hii inaitwa parafilia.

Mapenzi kati ya watu
Mapenzi kati ya watu wawili ni hisia za nguvu kuliko kumpenda mwingine kwa jumla. Mapenzi yasiyotuzwa ni hisia za mapenzi ambazo haziwezi kulipwa au kurudishwa. Mapenzi kama haya yanaweza kuwepo kati ya wanafamilia, marafiki, na wanandoa. Pia kuna matatizo kadhaa ya kisaikolojia yanayohusiana na mapenzi.

Katika historia, falsafa na dini ndizo taaluma ambazo zimewaza sana suala la mapenzi. Katika karne ya 20, sayansi ya saikolojia imeandika mambo mengi juu ya suala hili. Katika miaka ya karibuni, sayansi za saikolojia ya mabadiliko, biolojia ya mabadiliko, anthropolojia, sayansi ya nyuro na biolojia zimezidisha ufahamu juu ya mapenzi.

Mapenzi ni nini?/Msingi wa kisaikolojia
Saikolojia inaonyesha mapenzi kama jambo tambuzi na la kijamii.

Mwanasaikolojia Robert Sternberg alibuni nadharia ya miraba mitatu ya mapenzi akasema mapenzi yana vipengele vitatu tofauti: urafiki, kujitoa, na uchu. Urafiki ni aina ambayo watu wawili huambiana siri na mambo kadhaa kuhusu maisha yao binafsi. Kuwajibika, kwa upande mwingine, ni matumaini kuwa uhusiano huo ni wa kudumu. Aina ya mwisho na inayopatikana sana ni mvuto wa kingono au uchu. Mapenzi ya uchu ni kama yanavyoonyeshwa katika kupumbazwa kimapenzi pamoja na mapenzi ya kimahaba. Aina zote za mapenzi hutazamwa kama mchanganyiko tofauti wa vipengele hivi vitatu.

Mwanasaikolojia kutoka Marekani, Zick Rubin alijaribu kutumia saikrometiki. Kazi yake inasema kuwa mapenzi yamejengwa na vipengele vitatu: upendo, kujali na urafiki.

Kufuatia maendeleo katika nadharia za umeme, kama vile sheria ya Coulomb ambayo ilionyesha kuwa nguvu chanya na nguvu hasi huvutiana, milinganisho katika maisha ya binadamu ilifanywa, kama vile "vitu vilivyo kinyume kuvutiana." Katika karne ya 20, utafiti juu ya desturi ya mahusiano ya kingono miongoni mwa binadamu umepata kwa jumla kuwa jambo hili si kweli kukija ni tabia na watu kwa kawaida kuwapenda wale walio na sifa zinazofanana na zao. Hata hivyo, katika nyanja chache zisizo za kawaida na maalumu, kama vile mifumo ya kinga, inaonekana kwamba binadamu hupendelea binadamu ambao ni tofauti wao (mfano, walio na mfumo wa orthojoni), kwa kuwa jambo hili litasababisha kupata mtoto ambaye ana sifa bora za pande zote mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, nadharia mbalimbali za maingiliano ya binadamu zimebuniwa, na kuelezewa kwa kuzingatia upendo, mahusiano, maingiliano, na mivuto.

Baadhi ya mamlaka ya Magharibi hugawanywa katika vipengele viwili vikuu, chenye utu na chenye kujipenda. Mtazamo huu umewakilishwa na Scott Peck, ambaye kazi yake katika uwanja wa saikolojia ya matumizi ilitafiti fafanuzi za mapenzi na maovu. Peck anasema kuwa mapenzi ni mchanganyiko wa "wasiwasi kuhusu ukuaji kiroho wa mwingine," na kujipenda sahili. [13] Kwa pamoja, mapenzi ni shughuli, si hisia tu.

Baada ya maelezo haya kidogo, tunaamini utakuwa umejifunza Mapenzi ni nini, lakini usisahau kuchangia kwa kucomment hapo chini juu kuhusu mada yetu hii nzuri ya Mapenzi ni nini?