May 13, 2018

Mwanamke ndio mtu mwenye nguvu zaidi Duniani.

Moja jambo ningependa ulifahamu ni kuhusu Utafiti uliofanywa hivi karibuni ambao umeonyesha mazingira magumu kama yale ya njaa, milipuko wa magonjwa na utumwa, wanawake wanaweza kuishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume.

Wanawake wa Kiingereza huishi mpaka miaka 83.1 ukilinganisha na wanaume miaka 79.5, Scotland miaka 82.1 kwa wanawake na wanaume miaka 77.1.

Wasomi kutoka chuo cha Southern cha Denmark wamezitazama data kutoka katika matukio saba ya kihistoria ambapo watu walipitia mazingira magumu, ili kupata utofauti.

Masuala yaliyoangaliwa ni pamoja na njaa iliyoikumba jamii ya Ireland mwaka wa 1845-1849, maradhi ya surua na maisha waliyoyapitia watumwa wa Liberia waliokuwa wakirejea Afrika kutoka Marekani mwanzoni mwa karne ya 19.

Watafiti walibaini kuwa tofauti ya jinsia kwenye vifo vya watoto wachanga ”kulichangia sana” tofauti kati ya umri wa kuishi kwa wanawake na wanaume, ikionyesha kuwa ”watoto wachanga wa kike waliweza kuishi kwenye mazingira hatari kuliko watoto wachanga wa kiume”.

Wataalam hao wamesema tofauti ya homoni pia ni sababu ya kuwepo tofauti hiyo, mfano wanawake kuwa na homoni nyingi za kiume, kuna athari ya vichochezi wakati homoni za kiume , zikikutwa kwa wingi kwa mwanaume, kunaweza kuathiri mfumo wa kinga mwilini.