May 13, 2018

Tiba ya vipara yagundulika nchini Uingereza

Watafiti kutoka Uingereza wamegundua tiba mpya kwaajili ya watu wenye tatizo la kipara kichwani.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Manchester wameeleza kuwa dawa hiyo inakwenda moja kwa moja na kutibu matundu ya nywele hivyo kupelekea nywele kuanza kuota.

Dawa hiyo imetengenezwa kulenga protini ambayo inatajwa kusimamisha ukuaji wa nywele hivyo kusababisha kipara.

Kiongozi wa utafiti huo Dr Nathan Hawkshaw ameeleza kuwa tiba hii itasaidia sana watu wenye tatizo la nywele zao kukatika au kunyonyoka.