May 10, 2018

Usipoudumisha urafiki kwa mpenzi wako, atakuchoka mapema

Katika ulimwengu wa mahusiano urafiki umeonekana kuwa kiini cha uhusiano bora kati ya wapendanao. Kumbuka wakati ulipowaona wanandoa au wapenzi fulani kwa mara ya kwanza, waliokuvutia kutokana na hali ya upendo, heshima, na urafiki wa pekee ulioshamiri kati yao.

Ulijisikiaje? mpenzi wako ni rafiki bora Pengine swali la msingi ni kwamba, inawezekanaje baadhi ya wapenzi kuendelea kudumu katika mahusiano yao kwa furaha na upendo unaozidi kuongezeka kila kukicha, ni jambo gani hasa linalowapa hamasa ya upendo wa dhati katika dunia iliyojawa na changamoto nyingi hivi?

Pia ni jambo gani linalowafanya waridhike na hali zao? Majibu ya maswali haya na mengine yanayoweza kuendana nayo yanategemea zaidi kiini cha furaha katika mahusiano. Je, umewahi kujaribu kuwachunguza wapenzi wakiwa mgahawani? Unaweza kugundua mengi sana kwa kuangalia mwenendo wa ushirikiano wao.

Je, huwa wanakuwa katika hali ya kushindwa hata kutazamana, au kila mtu anakuwa bize na simu yake? Usipoudumisha Urafiki kwa Mpenzi Wako, Atakuchoka Mapema Je, huwa wanakula kimya kimya bila kusemezana? Ikiwa unawatazama wapenzi na ukagundua uwepo mdogo wa viwango cha ushirikiano na mwingiliano kati yao, basi tambua wazi kuwa ni jambo la nadra sana kuipata furaha katika penzi lao. Lakini ukibahatika kuitazama jozi ya wapenzi marafiki utajifunza jambo tofauti na lenye kuvutia sana:

Kwanza unaweza kuwaona wakiingia mgahawani kwa furaha katika hali ya uchangamfu na pengine wakiwa wameshikana mikono, hali wakishirikiana katika mazungumzo wakishirikishana uzoefu wao katika mambo mbalimbali, hata wakiwa wameketi, utawaona wakiangalia orodha ya vyakula (menyu) wakiambatanisha utani na vicheko vya furaha ndani yake, na kwa hakika wanapokula, Unaweza kuona muunganiko na mawasiliano yaliyopo kati yao, utabaini mtindo wa maisha ya pekee ya wapendanao wenye taswira ya moja kwa moja na upendo wa dhati. Watu wanapokuwa katika uhusiano wenye mapenzi ya dhati, huwa wana dhana ya umoja na urafiki ambao daima huashiria muunganiko wa kihisia wa hali ya juu.

Ikiwa unataka kurejesha uhusiano wako katika mstari ulionyooka, unapaswa kuanza kumtendea mpenzi wako kwa huruma na fadhili unazowapa rafiki zako wa karibu zinaweza kuwa na manufaa makubwa.Usipoudumisha Urafiki kwa Mpenzi Wako, Atakuchoka Mapema Yafuatayo ni mapendekezo muhimu ambayo yanaweza kukusaidia kurejesha uhusiano wa karibu na mpenzi wako:

Unapozungumza na mpenzi wako, zingatia maneno unayotumia, toni ya sauti yako, na mtazamo unao uonesha kwa mwenzi wako. Ikiwa ni maneno ambayo hayajengi na pengine hayakaribishi uhusiano wa kirafiki katika penzi lenu , unapaswa urekebishe mtindo wako wa mawasiliano. Fikiria ujumbe unaomtumia mpenzi wako. Je! Unamuonyesha mpenzi wako heshima kama vile unavyowaonyesha marafiki zako? Je, unapo muandikia ujumbe unajipa nafasi ya kuhakiki kama ujumbe uliouandika unamstahili?

Ikiwa hii inaonekana kuwa ni jambo ambalo ni la kawaida tena halina umuhimu wowote, fikiria kuhusu ujumbe unaopenda kuupokea kutoka kwa mpenzi wako, je ungependa akutendee kama vile umtendeavyo? Urafiki kwa Mpenzi Wako Atakuchoka Mapema Mtiemoyo mpenzi wako katika kile anachofanya pia jiepushe na tabia ya kukosoa juhudi zake.

Kama vile marafiki wanavyokutarajia kuwapa faraja na msaada, ndivyo anavyopaswa kumfanyia mwenzi wako. Hata kama huvutiwi na kazi yake, lakini tambua kuwa anahitaji msaada wako katika namna moja au nyingine. Ulimchagua huyo anza leo kumfaa kama unavyowafaa rafiki zako. Uwe mvumilivu na mwenye subira mpenzi wako anapokosea, hii ifanywe bila kujali uwezo wako wa hekima na ufahamu.

Mbona rafiki zako wanapokosea huwa unawatia moyo na kuwatendea kwa unyenyekevu hali ukiwaelekeza namna ambavyo walipaswa kutenda, kwanini usimtendee hivyo mwenzi wako? Tunapaswa kutambua kwamba kwa chochote tunachowatendea wapenzi wetu kina nguvu kubwa ya kuleta furaha au huzuni maishani mwao, na furaha inapokosekana, mambo mengi huathiriwa vilevile, ikiwemo suala nyeti la tendo la ndoa.

Mpenzi wako Jifunze kuwa sehemu ya furaha ya mpenzi wako kwa kuonyesha ushirikiano katika mambo yanayomfurahisha, kwa mfano; kama mwenzi wako anapenda vichekesho, mtandao wa internet umerahisisha mambo mengi, unaweza kutafuta video za vichekesho na ukazitazama pamoja naye. Kwa kufanya hivyo kwanza, unajenga urafiki na pili, unamsaidia aone uthamani wako kwake. Fahamu kinachomfurahisha na umpatie kwa kadri uwezavyo, atakuwa mpenzi rafiki!mpende mpenzi wako Epuka matarajio yasiyofaa.

Ikiwa kama unatarajia mpenzi wako awe anakuletea zawadi, anza kumletea zawadi pia, na hapa watu wengi hukosea sana kwa maana wengi huwapelekea wapenzi wao zawadi mara moja au mara mbili tu kisha wanaanza kulalamika “nampelekea zawadi kila siku lakini yeye hawezi kuninunulia hata pipi”, mpenzi wako ni binadamu sio robot hivyo anaweza kujifunza taratibu na sio haraka kama program za kompyuta, nikiwa na maana kwamba utatakiwa uendelee kumletea zawadi bila kuchoka ndivyo atakavyojifunza kukutendea kwa wema pia. mpenzi wako ni rafiki yako Epuka kutumia kauli za lazima, katika kumtaka mpenzi wako atekeleze wajibu wake.

Unapaswa kuchunguza uwezo wa utendaji na kikomo chake, itakusaidia kubuni njia bora za kumfundisha kwa utulivu. Kama unaweza kuwatendea rafiki zako kwa heshima, unashindwaje kumpa haki hiyo mpenzi wako?jali hisia za mpenzi wako Heshimu hisia na maamuzi yake. Ikiwa mpenzi wako ameamua kufunguka kwako, kwa kukueleza siri zake au kosa alilolifanya bila kukuweka wazi, heshima uaminifu wake na usimpige wala kutafuta sababu za kubatilisha uhusiano wenu. Kumbuka ameamua kufanya hivyo kwasababu anaamini wewe ni mtu sahihi kwake na hivyo unapaswa kujua mapungufu yake na ikiwezekana umpatie msaada wako.

Ikiwa kama umepokea malalamiko yanayomuhusu mpenzi wako, shughulikia tatizo lake kwa utulivu na kwa usawa, kama vile ufanyavyo kwa rafiki zako, kwa umakini na pengine ucheshi kidogo. Kumbuka: Tamaa ya mahaba na tendo la ndoa kwa ujumla ni sehemu muhimu ya uhusiano, lakini urafiki na ushirikiano ni tunu pekee ambayo inalifanya gurudumu la wanandoa lizidi kusonga mbele.