May 20, 2018

Wanaume wenye wanawake wanene huishi maisha marefu, yenye furaha.

Watalaam wa masuala ya utafiti wamekuwa wakijitahidi kufanya tafiti mbalimbali Duniani kote leo wamekuja na utafaiti mpya unaosema Wanaume ambao wana wachumba wanene huishi maisha marefu na  yenye furaha ikilinganishwa na wale wembamba.

Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na Dr. Filemon Alvarado na Dr. Edwagardo Morales katika chuo kikuu kimoja nchini Mexico. 

Aidha utafiti huo umeonesha kuwa wanawake wanene huwa wana ujasiri na mara nyingi hawakasiriki upesi.

Musyoka John ambaye ana mke ‘mwembamba’ ameeleza kuwa mara nyingi mkewe humhangaisha na hawana uhusiano mzuri katika ndoa yao.

Ameeleza kuwa mkewe anapoamua kufanya jambo ama kukataa, kamwe hawezi kugeuza msimamo wake.