June 7, 2018

Aina 6 ya vyakula vyenye kuongeza nguvu na kuimarisha kinga ya mwili

Unapozungumzia vyakula vyenye kuongeza nguvu na kuimarisha kinga ya mwili basi huna budi kwanza kuzingatia lishe bora na mpangilio mzuri wa ulaji kwani kila kitu kikizidi mwilini huwa ni tatizo.

Vyakula huvi husaidia kuimarisha kinga ya mwili pia husaidia kulinda mwili usipatwe na magonjwa. Vipo aina na hivi ni moja ya vyakula hivyo.

1.Yogurt ( Maziwa mtindi )
Unywaji wa maziwa ya mtindi husaidia kuweka mwili katika kinga ya magonjwa kama UTI, Fangasi na mengineo kwani maziwa hayo yanasaidia kuogeza Kinga ya mwili.

2. Matunda
Katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

3. Supu ya kuku
Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

4. Viazi vitamu
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

5. Samaki
Walaji wa samaki wapo katika kundi la kutopata magonjwa yanayosababishwa na hewa kwa ulaji wa samaki husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa.

6. Matikiti/Maji
Kwa kuwa tunda hili lipo katia asili ya kuwa na maji basi sio vibaya kuliweka hapo. Tikiti ni tunda ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilini, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.