June 5, 2018

China usipowatembelea wazazi unafungwa jela

Mwaka 2003 serikali ya China ilipitisha sheria inayosema kuwa “watu wazima wanatakiwa kuwatembelea wazazi wao mara kwa mara”.

Unaambiwa hivi mtu akikaidi sheria hiyo basi mahakama itampangia ratiba ya kuwatembelea wazazi wake kwa kipindi fulani kwa kila mwezi au atapigwa faini na pengine kufungwa jela.

Aidha sheria hiyo imetungwa kukabiliana na upweke wanaopata watu wenye umri wa juu baada ya watoto wao kuondoka nyumbani baada ya kuanzisha familia zao.

Kwa mujibu wa sheria hiyo pia watoto wanalazimika kuwajali wazazi wao katika kila Nyanja ikiwemo ya masuala ya kiroho.