June 10, 2018

Fahamu jinsi ya kupunguza uzito kwa kutumia maji

Maji ni uhai hii ni moja kati ya kaulimiu amabayo imekuwa ikizunguka maskioni mwa watu, lakini na naomba ni ongezee kauli mbiu nyingne ambayo inasema maji ni uhai lakini pia ni dawa.

Yapo magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kutibika kwa kunywa maji pekee. Miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na maumivu ya kichwa. Lakini pia maji husaidia sana kwa mtu amabye anataka kupunguza uzito kama endapo mtu huyo atazingatia yafuatayo;

1. Pindi tu unapoamka asubuhi- kunywa kati ya glasi mbili hadi tatu za maji

2. Baada ya saa moja (Kabla ya kifungua kinywa)-kunywa kati ya glasi moja mpaka mbili za maji (kati ya 250ml na 500ml)

3. Kila unapokunywa kikombe cha chai/kahawa-kunywa glasi moja ya maji .

4. Dakika ishirini (20) kabla ya kila mlo- Kunywa kati ya glasi moja  mpaka mbili za maji.

5. Masaa mawili (2) kabla ya kwenda kulala -Kunywa kati ya glasi mbili mpaka tatu Zaidi ya maji kukusaidia kupunguza uzito lakini vilevile yatakuwezesha kuwa na ngozi nzuri na nyororo. Jitahidi kubadili mfumo wa maisha yako na kufanya maji kuwa sehemu ya maisha yako na si tu kwa ajilli ya kupunguza uzito.