June 10, 2018

Fahamu kuhusu urembo wa kucha (mitindo mbalimbali)

Tunona kila siku ubunifu katika suala la urembo linazidi kukua, hasa urembo wa kucha wabunifu wamekuwa wakitafuta mbadala wa watu wasioweza kufuga kucha na kupendeza waweze kufurahi kucha zao.

Kuna aina mbalimbali za kupendezesha kucha, ila leo tutaangalia juu ya ubandikaji kucha, ambao umekuwa ukishamiri kila kukicha hasa kwa upande wa wanawake.

Ubandikanji kucha umekuwa ukifanyika kwa aina tofauti tofauti, ila cha msingi ni kutambua unapenda kucha zako ziwe katika muonekano gani, pia tambua rangi itakayo weza kuendana na ngozi yako ya kucha iliuvutie zaidi.