June 8, 2018

Mwanamke usipaniki yanapojiri mambo haya

Kumekua na hulka ya akina dada, hasa wa kizazi cha leo, akina mama sio sana pindi anaposikia kuwa mume wake amechepuka ataanza kuhisi mambo mengi, kama kujitoa kasoro, au kufikiria nini mume wake amekosa kwake, je hana uzuri wa kumvutia mumewe? Au kaamua kutoka kwa kua anamdharau nk,jibu rahisi ni kwamba unaweza usiwe na kasoro yoyote ile, tena yawezekana mchepuko wa mwanaume wako unaweza ukawa haukufikii wewe kwa lolote,

Wanaume kuchepuka ni hulka yao tuu hasa nchi zetu za kiafrika, tena mara nyingi wengi huwa hawana sababu ya msingi ya kufanya hivyo isipokuwa ni "just for new taste" na kuonyesha "identity na prestige" tuu na ndio maana wanaume wengi wanaochepuka huwa hawataki kabisa kuanza kuongea madhaifu ya mkewe kwa mpango wa kando wake, hii ni kuonyesha kuwa anaheshimu nyumbani kwake na hayuko radhi kuharibike.

Imekuja kuonekana miaka ya karibuni kuwa ni kikwazo hasa baada ya kuzuka harakati nyingi za "kumkomboa" mwanamke na mambo ya "haki sawa" kwamba kuwepo na nguvu sawa za kimamlaka ndio zimekuja kusababisha migogoro mingi na kutokuelewana miongoni mwa wanandoa siku za karibuni, kwamba baba akichepuka na mama lazima afanye hvyo.

Kwa bahati mbaya jamii imekua na hukumu tofauti kwa kosa moja lililotendwa na watu wa jinsia mbili tofauti kwa hyo dada zangu ukiona hari hyo inatokea usishangae sana wala kujiuliza una tatzo gani, kama una kasoro za kawaida zisahihishe ila walio wengi atatoka hata kama huna kasoro, chakufanya chukua hatua stahiki za kuendelea kuokoa mahusiano na kuendelee kumnasihi mwandani wako akumbuke familia na amuogope Muumba wake, wengi hua wanaelewa.

Muhimu: Sihamasishi wanaume kufanya hivyo, haifai.