June 8, 2018

Vitu hivi vitamfurahisha mwenzi wako muwapo pamoja nyumbani - Ladies.

Kumfanya mume wako aridhike kimapenzi maana yake ni kufanya akuangukie kimapenzi zaidi. Kufanya mapenzi kwa wanandoa ni njia nzuri ya kuwaunganisha kinafsi na kujipa raha na ukaribu.

Ukijifunza sanaa ya kumkaribisha na kuwa tender kwa mwenzako basi mnaweza kutengeneza bond ambayo ni strong na mume au mke atakufurahia siku zote za maisha yenu.

Kumfanya mwanaume awe na furaha kwa mke wake huonesha jinsi unavyompenda na pia inampa msukumo wa kuhakikisha anakuwa karibu na wewe kimahaba na kuwa na muda na wewe kama wapenzi.

Kuna vitu vingi ambavyo mwanmke huhitaji kufanya kwa mume wake hata hivyo kila mwanaume ana tofauti na mwingine na kila mwanaume ana ladha yake linapokuja suala la mapenzi au tendo la ndoa.

Hivyo ni jukumu la wewe mwanamke kujifunza na zaidi kufanya utafiti wa kutosha kujua mume wako anapenda kitu gani kwako na pia mwili wako upo sensitive wapi. Kila mwanaume hupenda kuona mke wake akionekana sexy na nguo zile amevaa, inawezekana mpo wawili tu yeye na wewe, kwa nini usimtanie mzee na kinguo cha uhakika kisha pima meter yake itasoma vipi?

Kuna vinguo vya kuogea, kuna vinguo vya chumbani, kuna nguo za kuvaa ofisini au kazini nk kila nguo huvaliwa mahali pake.

Huwezi kuvaa nguo ya kazini chumbani!
Unajua kuchezesha sauti pia kuna raha yake kumfanya mwanaume joka litoke pangoni, siyo kila siku kulalamika tu, lawama tu, manung’uniko tu, acha hizo jaribu siku hata kama anakosea kila siku anza kumsifia hata kwa vitu vidogo tu, mpe asante, mkumbatie na kumpa romantic touch, uwe mbunifu.

Siamini kama kuna mwanaume ameoa mke ambaye siku zote ni kelele au kununa tu, au kulalamika tu au kuongea tu makosa na kusahihisha, kwa nini asikukwepe, hata kama anakosa siku zingine geuza udhaifu wake kuwa kitu kizuri au uwe na mtazamo positive.

Hata siku moja hujamchezea kifua au kidevu chake, mfanye ajisikie yeye ni mwanaume special.
Mwanamke anatakiwa kumlinda mumewe na maadui wote kiroho na kimwili lakini wakati mwingine mke hujisahau na kuzoea ndoa hadi mume ana fall in love kihisia na mwanamke mwingine (nyumba ndogo).

Hata hivyo inawezekana mume huwa haja fall I love na yule mwanamke bali ame-fall in love na hisia zile wewe humpi na akikutana na huyo mwanamke anajisikia raha na kupata kile love tank yake ndani ya moyo wake huhitaji hata kama mwanamke mwenyewe hampendi ila emotionally ameoza kwa huyo mwanamke na anajikuta anavutwa na yeye badala ya wewe kumvuta.