August 10, 2018

Mambo 10 msingi ya kufuatilia unapokuwa unajiandaa na mitihani.

 MAMBO KUMI YA MSINGI YA KUFUATILIA UNAPOKUWA UNAJIANDAA NA MITIHANI
Swala la maandalizi kwa mwanafunzi katika kipindi hichi cha mwisho ni kitu muhimu zaidi ingawa kuna msemo umejijenga katika vichwa vya watu wengi “NG’OMBE HANENEPI SIKU YA MNADA” ndugu mwanafunzi kataa kabisa usemi huu kuuweka katika kichwa chako, hata mimi nilipokuwa mwanafunzi nilikataa kabisa msemo huu,mimi nilikuwa naamini kuwa “NG’OMBE ANANONA SIKU YA MNADA” (angalizo lakini sio kusoma kitu kipya mpaka dakika ya mwisho unaingia  kwenye chumba cha mtihani) na wewe pia amini ng’ombe ananona siku ya mnada.Hakuna kitu muhimu kama siku za mwisho za kujiandaa na mitihani yako,unaweza ukawa umejiandaa vizuri sana huko nyuma lakini kipindi kiki cha mwisho ukamaliza vibaya na kukupelekea kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yako.

Kipindi hichi cha mwisho ni kipindi cha utulivu, lakini pia nakuomba kama kuna mzazi au mlezi anasoma mda hii basi nomba wewe ndio uwe chanzo cha kufanya mwanao anapata utulivu,acha kumgombeza ovyo mtoto katika kipindi hichi na kumsema maneno makali ya kumfanya kukosa ule utulivu wa ndani,pia kama mwanao anakaa nyumbani hakai shuleni basi pia katika kipindi hichi naomba umtoe katika ratiba za kazi za nyumbani,mpe muda wa kutosha sio mtoto anarudi nyumbani basi jambo la kwanza kumwambia kuna vyombo vya kuosha vinakusibiri! Wiki hii mpe likizo mwache asome zaidi na apate muda wa kupumzika wa kutosha.

Mambo kumi ya kufuatilia katika kipindi hichi ni kama yafuatayo;

1. Kuwa mtu wa Sala au karibu na Mungu

Kwa mwanadamu wowote yule ni jambo la lazima kuwa mtu wa sala muda wote  ingawa maisha ya kudunia yanatusonga na kutufanya kumsahamu mwenyezi mungu na kuyashika ya dunia.Mwanafunzi hata kama umekuwa nyuma sana katika maswala ya kiimani basi hichi ndio kipindi cha kuwa karibu na mungu wako,ongea na mungu ,omba sana ,mwombe mungu akupe wepesi katika mitihani yako,mwombe mungu akulinde na yote mabaya yanayoambatana katika kipindi hichi cha mtihani maana ndicho kipindi amabcho kwa wanafuzi huwa yanazuka magonjwa na haijulikani yametokea wapi ,hayo magonjwa mara kichwa kinagonga,mara sioni vizuri basi ni kipindi cha kupigana na nguvu za  giza,mwombe mungu akuepushe na watu wabaya wanaotaka kuinuka katika kipindi hichi,omba utulivu,ule utulivu wa kutoka ndani,omba kumbukumbu yako vizuri ,ushindwe hali ya hofu,pia usijinee mabaya katika kipindi hichi.

2. Tumaina la kufaulu kuwa kubwa kuliko hofu ya kushindwa


Hakuna kitu kibaya kwa mwanadamu kama hofu tena hofu mbaya zaidi ni FEAR OF FAILURE .Hofu ya kushindwa ni tatizo kubwa kwa mwanadamu kuweza kufika malengo yake,wanafuzni wengi wanashindwa mtihani hata kabla hawajaingia katika chumba cha mtihani,wengi wao wanakuwa tayari wameshashindwa,mwanafunzi anakuwa tayari  ameshashindwa kutokana na hofu ,anajipima uwezo wake yeye mwenyewe na kujiona hawezi tena ,unakuta ni kipindi ambacho mwanafuzni anakumbuka mitihani yote aliyoshindwa  siku za nyuma na kujiona hawezi tena ,tena unakuta anajisemea moyoni “hii mitihani ya kawaida imenishinda ije kuwa huu wa taifa?” lakini kumbuka ujianavyo moyoni mwako ndivyo ulivyo vile vile hakuna kitu kibaya na kizuri kama ulimu wako,ulimi unalaani lakini pia ulimi unabariki,.katika kipindi hichi chakujiandaa wacha kinywa chako kijae ushindi,jione umeshashinda na sasa unasubiri muda tu wa kuingia kwenye chumba cha mtihani,kumbuka mitihani yote uliyofanya vizuri,kumbuka 90 zote ulizopata na jisimee mwenyewe kimomoyo ninakwenda kushinda sasa na kusonga mbele.

3. Sio kipndi cha kujifungia ndani peke yako na kukesha


Katika kipindi hichi cha mwisho cha kujiandaa na mitihani yako si kipindi cha kujifungia ndani peke yako na kujisomea ndani ,hichi ni pindi cha kujichanganya na wenzio tena wa shule mbalimbali.
Fanya sana group discusion ujue mambo usiyoyajua na mapungufu uliyonayo na kipi upo vizuri,hakuna njia rahisi ya kusoma na kukumbuka kitu kama kusoma kwa makundi hii itakuwezesha hata unapokuwa katika chumba cha mitihani kukumbuka kwa urahisi tena utakumbuka hata aliyetaja hio pointi wakati mpo kwenye discussion. Hata siku moja usiamini unajua kila kitu,jua kabisa kuna vitu unahitaji kupata kutoka kwa wengine ,kama baadhi ya vitu hujui wenzio wanajua ,pia kuna watu wengien ni mabingwa wa kuotea maswali,akisema hili lipo jua basi kweli utalikuta.

4. Yajue maeneo muhimu na kuweka nguvu kubwa

Hili pia ni jambo la msingi kujua wapi unatakiwa kuweka nguvu katika kipindi cha mwisho cha kujiandaa na mitihani yako ya mwisho ,katika kuweka nguvu unatakiwa kuweka mkazo katika mambo mawili

  a)   Yale msaomo ambayo unahakika unayajua vizuri na uelewa mkubwa
Mara nyingi kila mwanafunzi anakuwa na masomo ambayo anajua anafanya vizuri hivyo basi ni vizuri kuweka nguvu kubwa katika hayo masomo maana ndio yatanyanyua Division/GPA yako,hakikisha masomo ambayo unauwezo  nayo wa kufaulu hukosi chini ya B+ .Hakikisha unakufa nayo,jua hayo ndio mkombozi wako,lakini kumbuka pia unatakiwa kuweka nguvu pia kwenye masomo mengine pia maana usije pata A huku kwingine unapata F jua utashusha division/GPA yako maana matokeo yote huwa yanatafutwa kwa kwa kanuni ya LAW OF AVERAGE

   b)  Uliko na mapungufu na kuna maksi nyingi
Lakini pia lazima uweke nguvu kubwa kwenye sehemu yenye mapungufu ambayo unajua maswali yake yana maksi nyingi. Kipindi hichi cha mwisho lazima ujue ni eneo gani una mapungufu lakini nieneo ambalo linaulizwa sana kwenye mitihani ,hapa sasa ndio umuhimu wa kujua umuhimu wa kujua mfumo wa mtihani unavyokuja nitalielezea hili kwenye point inayokuja.Ukishajua mapungufu uliyonayo na wewe mwenyewe huwezi basi mtafute mwalimu au mwanafunzi mwenye uwezo nalo akupe msaada

5. Kurudia zaidi mtihani iliyopita na kujua muundo wa mitihani ilivyo

Mwezi wa mwisho ni vizuri zaidi mwanafunzi kupitia mitihani ya nyuma ya kutosha kuna material mengi yameandaliwa yenye mitihani toka ya mwaka 1980 au kuna vitabu vyenye maswali na majibu ya mitihani ya taifa toka miaka ya nyuma,kwa hiyo ni vizuri kupitia mitihani ya kutosha ili kujiweka fiti,kujua mitihani inakuja vipi na inajibiwa vipi hata kama watarudia maswali basi itakuwa faida kwako kama uliyapitia maana kufanya swali unalolijua tayari lina faida nyingi ndani ya chumba cha mtihani,kwanza itakuwezesha kupata maksi nyingi lakini pia itakuwezesha kutumia muda mdogo na hivyo kutumia muda mwingi kwenye maswali mengine hivyo kuongeza kiwango chako cha kufaulu.Lakini pia kama upo na rafiki yako mnaweza kujipima kwa kuchagua mtihani mmoja ,mwishoni mkabadilishana mkasahishiana kwa kuangalia majibu au mkapelekea mwalimu mkamwomba naamini

6. Hakikisha pia unapata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala

Hapa wanafuzi hugeuka kuwa bundi maana bundi tu ndio huwa anakesha usiku.Najua hichi ni kipindi cha kusoma sana lakini pia ni lazima ujipe muda wa kutosha wa kupumzika ili uweze kuutendea haki ubongo,unajua  uwezo wa mwanadamu wa kuelewa una masaa na ukizidisha hapo basi unakuwa huingizi tena ,unakuwa unasoma maandishi kama picha,lakini pia hakuna kitu muhimu  kama kulala muda wa kutosha,usipo lala muda wa kutosha unasababisha matatizo mengine kama msongo wa mawazo,uwezo mdogo wa kufikiri na kijifunza,ufanisi kuwa mdogo ,hivyo basi ni lazima uhakikishe unapata muda wa kupumzika na kulala katika hichi kipindi cha kujiandaa na mitihani,usigeuke kuwa ndege wakati wewe ni mwanadamu maana unaweza kuna msemo unasema MSULI TEMBO MATOKEO SISIMIZI.


 Wakati mwingiine unatakiwa uusikilize mwili , kama mwili na akili vimechoka pumzika ,hakuna ubingwa wa kukesha,na wakati umelala ni vizuri hakikisha kama una simu umezima ili kuepuka usumbufu wa kuamshwa wakati simu inaita au toa sauti ukiamka utazikuta missed call lakini pia wape taarifa watu waliopo karibu hutaki kuamshwa mpaka muda wako wa kuamka utakapofika wa kuamka ili uweze kupata usingizi mzuri  ukiamka unakuwa kiumbe kipya chenye nguvu mpya.

7. Hakikisha unakuwa na material na notes nzuri
Pia kwa mwanafunzi hakikisha  unakuwa na malighafi nzuri,kama ilivyo kiwandani ili uzalishe bidhaa yenye ubora ni lazima malighafi nzuri,hivyo basi kwa mwanafunzi unatakiwa kuwa na material mazuri ya kushiba katika kipindi hicho cha mwisho,kusanya material kwa wanafunzi wanaofanya vizuri unaowajua pia tafuta material katika zile shule zinazofanya vizuri

Inakuwaje unaona material kutoka shule nzuri inayofanya vizuri unaliacha tu linapita kirahisi rahis tu? Unaweza kusoma sana lakini ukasoma vitu sio sahihi baadae matokeo yakawa tofauti na msuli uliopiga.Asilimia kubwa ya wanaofeli pia ni kutokuwa na material sahihi,lakini pia hakikisha unapata yaliondikwa kwa lugha unayoielewa,maana waandishi wengine wanataka sifa kwa kufanya mambo kuwa  magumu.

8. Hakikisha unahudhuria vipindi nakusikiliza maelezo ya mwisho ya walimu

Katika kipindi hichi cha mwisho pia imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanafunzi wengi kutopenda kuhudhuria shuleni na kujifungia wanapokujuawao,lakini hichi ni kipindi kizuri pia kuhudhuria shuleni/chuo na kujua maelezo yoyote mtakayopewa lakini pia mwanafunzi asidharau mwalimu anaposema ana kitu cha mwisho anataka kufundisha ,huwezi jua kwanini mwalimu anataka kufundisha kipindi hicho,hivyo ni vizuri kwenda kusikilizana kujiona umetimilika,unaweza ukashangaa peke yako unasema mwalimu mbona hichi akufundisha lakini kila mtu akakushaangaa maana mwalimu alishakifundisha mwishoni,mara nyingi haya mambo huwa yanatokea.

9. Hakikisha kumbukumbu zako zinaongezeka kadri kuda unavyozidi kwenda

Hakikisha kumbukumbu za vitu vyote ulivyosoma unaongezeka jinsi muda unavyozidi kwenda na kukaribia kufanya mitihani,maana kwenye mitihani unaingia wewe kama wewe,hakikisha unapata muda peke yako mtulivu kusikokuwa na kelele ya aina yoyote unaanza kuangalia maswali unaanza kujijibu wewe mwenyewe kama vile kuna mtu anakuuliza au unawezakuwa unaandika kamani pointi unaandika kwenye karatasi,hii itakuwezesha kujua wapi kuna mapungufu hivyo kutilia mkazo zaidi katika hilo eneo ambalo unaona bado haupo sawa.

10. Andaa summary katika masomo yako

Hichi kipindi cha mwisho pia,ni kipindi cha kujiandalia summary za notes zako za kwenye madaftari na vitabu maana itafika mwisho wa siku utashindwa kusoma madaftari na vitabu vyote,hivyo basi yale mambo ya msingi yote yaweke kwenye summary hii itakuwezesha kurudia mambo mengi kwa muda mdogo,na hivi vitu utaweza kuvikumbuka kwa urahisi zaidi.
 

Kama wewe ni mwanafunzi na una hofu sana katika kipindi hichi cha kujandaa mwishoni au ni mzazi unataka ushauri kwa ajili ya mwanao basi unaweza kutupigia kwa hizi namba (255 655 043 443/+255 769 360 989.)

Facebook @Chief Hope  Ama Richard Edward

By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.